MTO KONGO

Mto wa Kongo (kati ya 1971 and 1997 uliitwa
Zaire) ni mto mkubwa wa Afrika ya kati. Ni mto
mrefu wa pili katika Afrika baada ya Nile.
Beseni ya Kongo pamoja na tawimito yake ni
eneo kubwa la pili duniani la msitu wa mvua.
Pia kiasi cha maji pamoja na ukubwa wa beseni
yake zina nafasiy a pili duniani baada ya
Amazonas huku Amerika ya Kusini.
Jina la mto limepatikana kutokana na Ufalme
wa Kongo uliokuwa dola kubwa katika Angola
ya Kaskazini na Kongo ya Magharibi wakati wa
karne 14-17 BK. Jamhuri zote mbili za Kongo
zimepata majina yao kutoka kwa mto.
Mto wa Kongo ni njia muhimu ya mawasiliano
na biashara kwa meli zinazoweza kusafiri mle
kwa kushirikiana na njia za reli penye
maporomoko mahali patatu.
Chanzo cha mto kipo karibu na mji wa
Lumbumbashi katika jimbo la Katanga . Kwenye
kilomita 1,800 za kwanza mto unaitwa Lualaba .
Jina la Kongo latumiwa kuanzia mji wa
Kisangani ambako mto umepita maporomoko
ya Bayoma. Kuanzia Kisangani hadi Kinshasa
mto ni njia ya maji inayopitiwa na meli za
mtoni. Upande wa Lualaba kuna sehemu
kadhaa zinazofaa kwa meli lakini njia ya maji
inakatwa mara kadhaa na maporomoko..

Pia mto huu unapita katika misitu minne yenye mvua karibia vipindi vyote vya mwaka. Mto huu ni wa pili kwa upana duniani baada ya mto Amazon wa America ya kusini,wa pili kwa urefu barani  Africa  baada ya mto Nile na wa kwanza kwa kina kirefu duniani. Mto huu una samaki wakubwa sana wenye meno(kama inaonekana pichani) samaki hao huitwa Tiger fish..

TUNAJIVUNIA KUZALIWA KWENYE BARA LENYE MAAJABU

Share on Google Plus

About Wonders africa

0 maoni:

Chapisha Maoni